loader
Dereva bajaji jela miaka 30 kumpa mimba mwanafunzi

Dereva bajaji jela miaka 30 kumpa mimba mwanafunzi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya imemhukumu dereva wa bajaji kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumnajisi na kumsababishia ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne.

Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Andrew Scout alimhukumu kijana huyo mkazi wa Veta Machinjioni jijini Mbeya, Deus Peter (25) baada ya kukiri makosa katika mashitaka mawili.

Wakati akisoma mashitaka kwenye kesi hiyo namba 59 ya mwaka huu, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Hebel Kihaka akisaidiana na Wakili Zena James alisema Peter ni dereva bajaji. Wakili Kihaka alidai kuwa, kwa nyakati tofauti kati ya Septemba mwaka jana na Aprili mwaka huu, mshitakiwa alimnajisi mwanafunzi wa shule ya sekondari jijini Mbeya. Ilidaiwa mahakamani kuwa mwanafunzi huyo ana umri wa miaka 16 na kwamba kitendo cha mshitakiwa ni kinyume na kifungu namba 130(1) (2)(e) na 131 (1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Katika shitaka la pili kijana huyo alidaiwa kumsababishia ujauzito mwanafunzi huyo kosa ambalo ni kinyume na kifungu cha 60 A (3) cha cha sheria ya elimu ya (sura ya 353).

Upande wa mashitaka uliiomba mahakama itoe adhabu kama sheria inavyoelekeza ili iwe fundisho kwa mshitakiwa na watu wengine.

Mshitakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa anategemewa na kwamba hilo ni kosa la kwanza na anajutia alichokifanya. Hakimu Scout alimhukumu Peter kutumikia kifungo cha miaka 30.

foto
Mwandishi: Na Joachim Nyambo, Mbeya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi