loader
Watumishi wa umma wasisitizwa uadilifu

Watumishi wa umma wasisitizwa uadilifu

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa amewataka watumishi wa umma kuwa na utamaduni wa kufanya kazi kwa uadilifu bila kushinikizwa wakati wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kama ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza.

Mchengerwa alitoa wito huo jana ofisini kwake, wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliolenga kutoa mrejesho wa masuala ya kiutumishi yaliyojitokeza wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya hivi karibuni katika mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu. Alisema Rais amedhamiria kuwa na watendaji waadilifu, hivyo ofisi yake imejipanga kuhakikisha watumishi wote wa umma wanasimamia vema fedha zinazotolewa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

“Inawezekana wapo baadhi ya watumishi wanataka kutekeleza wajibu wao kwa kushinikizwa jambo ambalo Rais halitaki kwani anataka kila mtumishi awajibike bila kusimamiwa,” alisema.

Aidha, aliwataka watumishi wa umma nchini kuzingatia maelekezo ya Rais Samia kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Covid-19 aliyoyatoa Oktoba 10, mwaka huu.

Waziri Mchengerwa alisema watumishi wa umma waliopewa dhamana ya kusimamia miradi, wanapaswa kutekeleza kwa weledi na uzalendo kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/e46ce500fcaa4a21801721f245dea790.jpeg

BODI ya filamu Tanzania imesema maandalizi ya tuzo za ...

foto
Mwandishi: NA MWANDISHI WETU

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi