loader
Dstv Habarileo  Mobile
Makanisa nchini yakataa akanisa nchini yakataa matangazo ya ndoa za utotoni

Makanisa nchini yakataa akanisa nchini yakataa matangazo ya ndoa za utotoni

MATANGAZO ya ndoa za wasichana walio chini ya miaka 18 sasa hayafi kishwi makanisani kutokana na juhudi zinazofanyika kupinga ndoa za utotoni katika Kata ya Mpwayungu Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.

Hayo yalibainika juzi wakati wa mkutano wa kujadili Mpango Kazi wa Taifa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA). Mpango huo uliandaliwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali la Women Wake Up (WOWAP) na kushirikisha kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto ngazi za kata na vijiji vya Mpwayungu, Chikola na Nagulo, Wilaya ya Chamwino.

Mtendaji wa Kijiji cha Mpwayungu, Selemani Kibakaya alisema sasa hakuna taarifa za kuripotiwa kwa ndoa za mabinti chini ya miaka 18 ambazo matangazo yanapelekwa kanisani kwani mapadri na wachungaji wamekuwa wakiyakataa.

Kibakaya alisema ndoa za utotoni ambazo ni chini ya miaka 18 huwa hazitangazwi kanisani, zinapingwa katika kata, sehemu za ibada mtu kwenda kuandikisha ndoa chini ya miaka 18 hairuhusiwi. Alisema sasa jamii imekuwa na uelewa na imekuwa ikitoa taarifa juu ya vitendo vya ukatili ikiwemo ndoa za utotoni.

Pia alisema umasikini umefanya baadhi ya wazazi kufumbia macho watu waliowapa mimba binti zao wenye umri mdogo. “Mtoto anabakwa anapewa mimba mzazi anapewa Sh 200,000 fedha ambazo hajawahi kuzishika tangu azaliwe anakubali na kesi inaishia hapo na mzazi ukimfuata anasema mtoto si wa kwangu kwani kuna shida gani katika hali kama hiyo hawezi kutoa ushirikiano,” alisema.

Shehe wa Kata ya Mpwayungu, Nurdin Ndunguru alisema kamati za MTAKUWWA zinafanya kazi kubwa ya kufuatilia ukatili unaofanyika katika jamii. “Lakini bado kuna baadhi ya watu wanatetea uhalifu, mhalifu anakuja kukusuta mtaani, kesi inakwenda Polisi lakini hakuna kinachoendelea, ukatili huu unamalizwaje wakati watu wanakamatwa na hawachukuliwi sheria,” alisema. Ofisa wa Polisi, Emmanuel Maduma kutoka Kituo cha Polisi cha Mpwayungu, alisema kuna matukio ya ukatili yanayoripotiwa kama vile ubakaji, kuwapa mimba wanafunzi na shida iliyopo ni ushirikiano kati ya wazazi na vyombo vya dola.

Alisema kati ya matukio 10 ni matukio mawili au matatu huwa na ushirikiano. “Unaletewa kesi ya ubakaji, tukio limetokea siku nne hadi tano ukiandika ripoti hata ushahidi unapotea, angewahi daktari angempima angekutana na michubuko na mbegu, vingesaidia kwenye ushahidi,” alisema.

Pia alisema kumekuwa na mazungumzo na wazazi wakishakubaliana wanakuwa na taarifa tofauti. “Ni jamii ambayo inakubaliana na inashirikiana na hawako tayari kumtaja mhalifu, ukimuuliza binti atakuambia kulikuwa na fundi anajenga hapa katokea Iringa ndiye aliyempa ujauzito, ukiwauliza namba ya simu wanasema hawana,” alisema.

Pia hati za wito kuwafikia walengwa imekuwa changamoto kutokana na mashahidi wengine kutofika kutokana na changamoto ya umbali na ukosefu wa nauli hali inayofanya kesi nyingi kufutwa.

foto
Mwandishi: Na Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi