loader
CDC yashauri taifa kujizatiti kukabili corona

CDC yashauri taifa kujizatiti kukabili corona

MKURUGENZI wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (CDC), Dk John Nkengasong ameshauri nchi za Afrika kujizatiti katika mikakati ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19, ikiwa ni pamoja na kupanua uwezo wa uchunguzi, kutengeneza chanjo na tiba.

Akitoa mada ya ‘Nafasi ya Afrika katika kukabiliana na ugonjwa huo’, Dk Nkengasong alisisitiza hitaji la nchi kukuza na kuimarisha taasisi za kitaifa za afya, kupanua uwezo wa utengenezaji wa chanjo, uchunguzi na tiba ili kuimarisha maendeleo ya nguvu kazi katika afya ya umma. Alisema ni vyema ikatumia mikakati ambayo itaongeza dhamira ya Afrika katika kukabiliana na changamoto zilizoletwa na janga hilo.

“Janga la Covid-19 limeonesha hitaji la sisi sote kujenga mifumo thabiti, kuzibadilisha, ili waweze kukabiliana na mwenendo wa Karne ya 21,” alisema. Pia alisisitiza hitaji la nchi za kiafrika kuwekeza katika mifumo yao ya afya ya umma, kujenga ushirikiano madhubuti na wa vitendo na mashirika ya ndani, sekta binafsi na mashirika ya kimataifa.

Meneja wa Mradi wa HPSSTuimarishe Afya unaotekelezwa na Shirika la Swiss TPH, Ally Kebby alisema kupitia kongamano hilo wamepitia maeneo ya msingi katika kuimarisha mfumo wa afya likiwemo suala lenye changamoto la dawa hususani katika ugavi na menejimenti ya dawa.

“Mradi wetu tumekuwa tunashirikiana na serikali kuimarisha mfumo wa afya kupitia afua mbalimbali kwenye sekta ya afya hususani kwenye bima ya afya ambapo tunashirikiana katika utekelezaji wa CHF iliyoboreshwa,” alisema.

Zaidi ya wadau 600 wa afya wakiwemo watunga sera, wawekezaji wa huduma za afya, wanasayansi, wamiliki wa hospitali na mashirika yasiyo ya kiserikali ya ndani na ya kimataifa, wamekutana kuangalia kwa kina mustakabali wa huduma ya afya Tanzania, iliyoongozwa na kaulimbiu ‘Hakuna kumuacha mtu nyuma 2021-2026’

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/446b2864245158003f38660343cbd2dd.jpeg

DROO ya 8 ya Kampeni ya 'NMB Bonge ...

foto
Mwandishi: Na Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi