loader
Dstv Habarileo  Mobile
Serikali inakamilisha vigezo Chato kuwa Mkoa

Serikali inakamilisha vigezo Chato kuwa Mkoa

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu amesema Serikali inakamilisha vigezo vitakavyoruhusu Wilaya ya Chato, iliyopo mkaoni Geita, kuwa Mkoa.

Rais Samia amezungumza hayo leo, Oktoba 14, 2021 katika kilele cha mbio za Mwenge, hafla iliyofanyika katika Uwanja wa Magufuli uliopo Wilaya ya Chato, mkoani Geita.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya ukaguzi wa miradi mbalimbali, na kiongozi wa mbio za mwenge, Luteni Josephine Mwambashi, Rais Samia amesema bado wilaya hiyo haijawa mkoa, ikiwa kama utakidhi vigezo, rasmi utakuwa Mkoa.

 Aidha, Rais Samia amesema kuwa Serikali imepanga kukamilisha miradi yote iliyopo wilayani humo ukiwepo mradi wa ujenzi wa Msikiti uliokuwa ukitekelezwa na Hayati Dk John Magufuli.

 Miradi mingine ni Bandari ya Nyamirembe, Uwanja wa Ndege wa Chato, Hospitali ya Wilaya, Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) na stendi.

"Nafahamu yapo mambo ambayo Hayati Magufuli aliwaahidi Wana Chato wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 ikiwemo upanuzi wa Bandari, kukamilisha ujenzi wa Uwanja wa Ndege Chato, Hospitali ya Wilaya, VETA pamoja na Stendi, nawahakikishia miradi yote itatekelezwa"Rais Samia.

foto
Mwandishi: Na Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi