loader
Dstv Habarileo  Mobile
Temesa waanza ujenzi wa jengo la abiria Mwigobero

Temesa waanza ujenzi wa jengo la abiria Mwigobero

MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi amepongeza Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) kwa kuanza ujenzi wa eneo la kupumzikia abiria na vyoo kwenye Mwalo wa Mwigobero mjini Musoma.

Licha ya pongezi hizo, RC Hapi hakuafikiana na taarifa iliyotolewa na Kaimu Meneja wa TEMESA wa mkoa huo Vitalis Bilali, kwamba mpaka ujenzi huo ukamilike utagharimu jumla ya Tsh milioni 89.

“Tundu Moja la choo serikalini linajengwa kwa Tsh  milioni 1·2 hapa mnajenga matundu manne sawa na milioni 4.8,”amesema RC.

 

Akishirikiana na fundi mkuu wa mradi huo, Mhandisi Joseph Elias, Hapi alifanya hesabu za haraka na kubaini kuwa gharama iliyotajwa ni kubwa ikilinganishwa na bei halisi za vifaa na ufundi.

“Ninafahamu michoro na gharama  umeletewa na wakubwa zako,  kawaambie wapitie upya hesabu ili gharama ipungue lakini mradi ukamilishwe kwa wakati huku mkizingatia ubora na thamani ya fedha,” amesema RC Hapi.

Agosti Mwaka huu, RC Hapi alifanya  ziara kwenye mwalo huo na kubaini  kukosekana kivuli kwa ajili ya abiria kusubiri usafiri pamoja na ukosefu wa huduma za vyoo.

Aliagiza muda wa mwezi mmoja kwa TEMESA kuanza ujenzi wa banda hilo na kuweka huduma zote muhimi kwa wasafiri ikiwamo za vyoo

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi