loader
Rais Samia aahidi kutatua changamoto za wananchi

Rais Samia aahidi kutatua changamoto za wananchi

RAIS Samia Suluhu Hassan leo amezindua Barabara ya Sanya Juu, Elerai mkoani Kilimanjoro, na kuahidi kuwa Serikali yake imejipanga kutatua changamoto zote zinazowakabili wananchi.

Amesema ahadi yake kama Rais na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ni kuangalia changamoto za wananchi na kuzifanyia kazi.

Rais Samia amesema barabara hiyo ilikuwa kero ya siku nyingi, ambapo ujenzi wake umekuwa wa awamu, na kuwa awamu iliyobaki ni kilometa 44 ambazo nazo usanifu umeshakamilika.

Amebainisha kuwa barabara hiyo ni moja ya ahadi katika Ilani ya Uchaguzi. Changamoto nyingine alizogusia ni pamoja na upatikanaji wa maji na migogoro ya ardhi ambazo pia ameahidi kuzitatua.

Amewataka viongozi wa maeneo hayo kushirikiana na serikali kuu kutatua changamoto za wananchi.

Rais Samia amewaomba wananchi kudumisha amani na utulivu, ili Serikali ipate wasaa wa kufikiri wapi itapata fedha ili kumaliza changamoto zinazo wakabili wananchi wake.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi