loader
Rais Samia kushughulikia changamoto ya Ardhi, Maji – Kilimanjaro

Rais Samia kushughulikia changamoto ya Ardhi, Maji – Kilimanjaro

RAIS Samia Suluhu, ameahidi kutatua changamoto ya migogoro ya ardhi inayoukabili mkoa wa Kilimanjaro kwa sasa.

Amesema changamoto zote ambazo ameziona kupitia mabango yenye ujumbe nyingi ni za migogoro ya ardhi, maji na maslahi ya watumishi huku akiahidi kwamba, atazichambua na kuzipatia ufumbuzi.

Ameyasema hayo leo akizindua barabara ya Sanya Juu - Elerai iyojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 32.2 na kugharimu kiasi cha sh bilioi 62.7

"Tunapita kuangalia yaliyotendeka na kuona changamoto zilizopo na hapa naona mabango mengi, kuna migogoro ya ardhi na maslahi ya wafanyakazi naomba tuyakusanye halafu tutakwenda kuyafanyia kazi.

"Changamoto hizi tutakwenda kuzifanyia kazi na  ahadi yetu CCM ni kuangalia kero za wananchi na kuzifanyia kazi," amesema Rais Samia na kuongeza:

"Najua hapa Kilimanjaro kuna changamoto ya maji na migogoro ya ardhi ambayo ndio kubwa zaidi na zote hizi nimeziona kwenye mabango hivyo, nitazichukua kwenda kuzichambua na kuzifanyia kazi."

Hata hivyo, Rais Samia amesema wapo baadhi ya wananchi waliojenga kwenye maeneo ya Serikali na wametakiwa kuondoka hivyo, ataangalia namna bora ya kushughulikia changamoto hiyo na kuipatia ufumbuzi.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi