loader
Dstv Habarileo  Mobile
Biashara yatakata Dar

Biashara yatakata Dar

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho, Biashara United, wameanza vema nyumbani baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Al Ahly Tripoli kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam jana.

Mabao ya Biashara kwenye mchezo huo yalifungwa katika dakika ya 39 na mshambuliaji Deogratias Mafie kwa shuti kali akimalizia vema pasi ya Denis Nkane, ambaye aliunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu wa Ramadhan Chombo.

Bao la pili katika mchezo huo lilifungwa dakika ya 60 kupitia kwa mshambuliaji kiongozi, Atupele Green, kwa shuti kali la nje ya eneo la 18 lililomshinda kipa wa Al Ahly.

Kocha wa Biashara United, Patrick Odhiambo, alifanya mabadiliko ya kiufundi dakika ya 36 kwa kumtoa Prosper Mushi na nafasi yake kuchukuliwa na Denis Nkane, lakini matokeo yalibaki hivyo mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Al Ahly wakiliandama lango la Biashara katika dakika ya 49 lakini uimara wa safu ya ulinzi ulizima shambulizi hilo. Dakika ya 57, kocha Odhiambo, alimpumzisha Mathew Odongo nafasi yake ikachukuliwa na Ibrahim Ndunguri.

Al Ahly walifanya mabadiliko katika dakika ya 58 kwa kumtoa Mohamed Makkari aliyempisha Ali Abu huku Abdulrahman Abusnina nafasi yake ikachukuliwa na Abdulrauf Alshoushan.

Biashara United, waliandika bao la pili katika dakika ya 60 kupitia kwa mshambuliaji kiongozi, Atupele, kwa shuti kali lililomshinda kipa wa Al Ahly.

Dakika ya 84, Biashara United walifanya mabadiliko ya kumtoa Atupele na nafasi yake ikachukuliwa na Notikely Masasi.

Timu hizo zitarudiana mjini Tripoli Libya baada ya wiki moja, na mshindi atasubiri timu itakayoshindwa kwenye Ligi ya Mabingwa kucheza nayo hatua inayofuata kabla ya kuingia makundi.

Katika hatua nyingine, wawakilishi wengine wa michuano hiyo Azam, leo watakuwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi kumenyana na Pyramids ya Misri.

Mechi hiyo inatarajiwa kuwa kali kutokana na ubora wa timu zote. Pyramids iliwahi kuja nchini kucheza na Yanga mwaka na kuiondomashindanoni.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/3c1aaaa05ecfe11db5ee008924757eb6.jpeg

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi