loader
Serikali kutoa 100% ujenzi jengo la mihonzi

Serikali kutoa 100% ujenzi jengo la mihonzi

SERIKALI imeahidi kutoa kiasi cha Sh bilioni 4 kugharamia ujenzi wa jengo la kutolea huduma za tiba ya saratani kwa mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) iliyopo Moshi mkoani Kilimanjaro.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema tayari serikali imekweshatoa Sh bilioni 1 na kiasi kingine kama hicho kitatolewa muda wowote kama sehemu ya kugharamia ujenzi wa kituo hicho.

Akizungumza katika maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50 ya Hospitali hiyo, Rais Samia pia amesema anatambua uhaba wa Watumishi na kwamba uchumi ukikua serikali itaongeza Watumishi.

 

“Inasikitisha kuona kwamba kwa miaka minne nyuma Hospitali ya KCMC haikuwahi kupata Watumishi kwa hiyo niwahakikishie kwamba tutakapopata upenyo wa kuajiri tutahakikisha KCMC nayo inapata fungu lake la Watumishi,” Rais Samia Suluhu, maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50 ya Hospitali ya KCMC, mkoani Kilimanjaro

Amesisitiza Serikali itaendelea kuiwezesha KCMC kuboresha miundombinu yake ikiwa ni pamoja na kuiwezesha kuweka mtambo wa kuzalisha mitungi tiba (oksijeni) wenye thamani ya Sh milioni 800, mtambo huu una uwezo wa kuzalisha mitungi 400 ndani ya saa 24.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi