loader
Rais Mwinyi atunuku vyeti askari 716, aonya kuepuka vitendo vinavyotia doa jeshi la Polisi

Rais Mwinyi atunuku vyeti askari 716, aonya kuepuka vitendo vinavyotia doa jeshi la Polisi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi kwa niaba ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu, leo Oktoba 16, 2021 amewatunuku vyeti na kuwapandisha vyeo Askari wahitimu 716 wa mafunzo ya Uongozi ngazi ya Sajini (SGT).

Rais Dk. Mwinyi amewataka askari waliohitimu mafunzo kwenda kufanya kazi na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya kazi ya uaskari ikiwa ni pamoja na udhibiti wa siri na uadilifu.

“Jiepusheni na vishawishi mbalimbali vinavyoweza kulitia doa Jeshi la Polisi na nchi yetu. Askari ni Kioo cha Jamii, Kwa hivyo mkiwa kazini na ndani ya jamii askari polisi awe ni mfano wa tabia njema na kutii sheria za nchi” amesema Dk  Mwinyi.

Aidha, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea uwezo watendaji ili wakatekeleze majukumu yao ipasavyo katika kuilinda nchi na mipaka yake pamoja na kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli zao za kiuchumi na kijamii katika hali ya usalama na utulivu.

Mahafali hayo yamefanyika katika Chuo cha Maafisa Polisi Kidatu, mkoani Morogoro na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, George Simbachawe

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi