loader
Kocha Simba: Tulieni kazi bado kwa Mkapa

Kocha Simba: Tulieni kazi bado kwa Mkapa

Kufuatia ushindi wa mabao 2-0 , walioupata Simba jana kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kocha wa timu hiyo Didier Gomes amewataka wachezaji wake wasishangilie sababu bado wanakazi nzito yakufanya kwenye mchezaji wa marudiano. 

Gomes amesema dakika 90, za Gaborone walizitumia kwa akili kubwa sababu alitambua wanacheza ugenini  hivyo wanatakiwa kujilinda zaidi huku wakishambulia kwa kuwastukiza. 

"Niwapongeze wachezaji wangu kwa kufuata viziri maelekezo niyowapa lakini furaha yao haitakiwi kuwa ya muda mrefu sababu bado tunakabiliwa na mechi ya marudiano hivyo nilazima tujiandae vyema ili mchezo wa marudiano tupate ushindi mkubwa na kuonesha ubora tuliliwa nao Simba,  amesema. 

Aidha Gomes amesema ushindi wa jana umempa matumaini ya kuipeleka hatua ya makundi kama ilivyokuwakwa msimu ulipita

Endapo Simba itashinda mchezo wa marudiano itafanikiwa kufuzu hatua ya makundi ambayo itakuwa ni mara ya tatu kwa misimu ya hivi karibuni lakini itakuwa ni mara yao ya pili mfululizo baada ya msimu uliopita kufanya hivyo kabla ya kutolewa na Kaizer Chiefs

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/336fdf21aeefbd12168518ee2b95b9f1.jpg

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi ...

foto
Mwandishi: Na Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi