loader
Kocha Yanga: Tunakuja kivingine

Kocha Yanga: Tunakuja kivingine

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasriddine Nabi amesema mchezo wa kesho dhidi ya KMC utakuwa na utofauti mkubwa na mechi mbili za ligi walizocheza. 

Yanga iliyopo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu kesho itakuwa mgeni wa KMC kwenye dimba la Majimaji Songea.

Kocha huyo amesema anajua ugumu wa mchezo huo ndio maana amesafari na jeshi lake lote lengo ni kuhakikisha wanarudi na pointi zote tatu ili kuendelea kujiweka kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo. 

"Naiheshimu KMC ni miongoni mwa timu ambazo zimefanya ussjili mzuri msimu huu na licha ya kutopata matokeo kwenye mechi zao mbili zilizopita lakini siwezi kuwadharau ninachojua mchezo utakuwa mzuri na mgumu kwa kila upande lakini sisi Yanga tunazihitaji pointi tatu, " amesema Nabi. 

Kwaupende wake kocha wa KMC Habibu Kondo, amekiri kwamba mchezo huo utakuwa mgumu sababu wanakutana na timu yenye mabadiliko makubwa ya kiuchezsji na mbinu.

"Hatuwaogopi Yanga lakini mchezo utakuwa mgunu lakini tumejiandaa kuhakikisha tunaanza ligi kwa kupata ushindi wa kwanza msimu huu mbele ya Yanga, wachezaji wangu wote wapo vizuri, " amesema Kondo.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/90506dbb41f4ec00e0ac7fc179f366c4.jpg

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi ...

foto
Mwandishi: Na Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi