loader
Matembezi kumuenzi bibi Titi kuzinduliwa kesho

Matembezi kumuenzi bibi Titi kuzinduliwa kesho

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kesho  atazindua matembezi ya vijana 3500 kutoka Dar es Salaam kuelekea Rufiji, Pwani kwa ajili ya kumuenzi Bibi Titi Mohamed ambaye ni mwanamke shujaa na jasiri katika harakati za ukombozi wa Tanganyika aliyefariki Novemba 5,  mwaka 2000.

Aidha matembezi hayo yanaenda sambamba na kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na jitihada zake za kuongoza taifa la Tanzania ikiwa ni miezi sita sasa.

Katibu wa Taasisi ya Bega kwa Bega na Mama, Fatma Sarhan alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari ambao ulizingumzia matembezi hayo ya siku tatu.

Alisema matembezi hayo yatahusisha taasisi hiyo kwa kushirikiana na wanachama wa Jogging Klabu za Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na waendesha boda boda kwa kutembea siku tatu kuanzia Mnara wa Mashujaa Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam hadi Ikwiriri wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani.

“Baada ya kuondoka Kongowe kutakuwa na vituo vitatu vya mapumziko, matembezi yatapumzika na kulala katika Kijiji cha Mwarusembe Wilaya ya Mkuranga, siku inayofuata watalalakatika Kijiji cha Njopeka katika Wilaya ya Mkuranga ambapo Oktoba 21 na 22 watalala katika Vijiji vya Bungu A na Kibiti katika Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani,” alisema.

Alisema matembezi hayo yataishia kijiji cha Ikwiriri wilaya ya Rufiji Oktoba 23, ambapo kutakuwa na shughuli mbalimbali zilizoandaliwa na UWT katika uwanja wa Mashujaa Ikwiriri.

Alisema Bibi Titi atabaki kuwa alama na nguzo muhimu ya mafanikio ya mwanamke nchini.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Madereva na Pikipiki Tanzania, Edward Mwanisongole alisema wanashiriki kwenye matembezi hayo kumuenzi shujaa huyo katika harakati za ukombozi.

Mwanisongole alisema pia wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapunguzia faini za makosa ya barabarani kutoka sh 30,000 mpaka 10,000 pamoja na changamoto ya kuingia katikati ya jiji lakini sasa wenye bodaboda wanaingia na kufanya shughuli zao kwa uhuru.

 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/cf4152d63831cf7b084abe5ae87d7749.jpg

BODI ya filamu Tanzania imesema maandalizi ya tuzo za ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi