loader
Udumavu wapungua, viribatumbo waongezeka

Udumavu wapungua, viribatumbo waongezeka

TAASISI ya Chakula na Lishe Tanzania (TFCN), imesema udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano umepungua lakini tatizo la uzito uliozidi na viribatumbo limeongezeka.

Mkurugenzi Mtendaji wa TFCN, Dk Germana Leyna amesema kuwa udumavu kwa watoto ulipungua kwa asilimia 34.7 mwaka 2014 hadi asilimia 31.8 mwaka 2018.

Dk Leyna, amesema tatizo la uzito uliokithiri kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa limeongezeka kutoka asilimia 29.7 mwaka 2014 hadi asilimi 31.7 mwaka 2018.

Alisema Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Mbeya na Unguja Mjini Magharibi inaongoza kwa tatizo hilo.

“Uzito uliokithiri ni chanzo kikuu cha magonjwa sugu yasiyoambukiza yanayaosababishwa na ulaji duni pamoja na mtindo mbaya ya maisha japokuwa tunajatahidi kupunguza tatio la udumavu na utapialo kuna tatizo hilo la ongezeko la uzito uliokithiri na kiribatumbo.

Alisema licha ya tatizo la udumavu kupungua nchini, bado kuna mikoa ambayo inakabiliwa na changamoto hiyo ya udumavu kwa watoto ikiwemo Mikoa ya Dar es Salaam, Kagera, Kigoma, Mara, Dodoma, Geita,Tanga, Ruvuma, Mbeya ,Morogoro na Tabora.

Dk Leyna alisema kiwango cha ukondefu kimepungua kutoka asilimia 3.8 mwaka 2014 hadi asilimia 3.5 mwaka 2018 lakini pamoja na kupungua kwa kiwango hicho bado kuna watoto 600,000 wanautapia mlo mkali na wa kadiri.

 

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi