loader
Gwajima ataka watanzania waishio ughaibuni kukumbuka nyumbani

Gwajima ataka watanzania waishio ughaibuni kukumbuka nyumbani

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima amewataka Watanzania wanaoishi na kusoma nchini Urusi kutumia fursa zilizopo Tanzania katika kuwekeza na kuwasaidia Watanzania.

Dk Gwajima ameyasema hayo jijini Saint Petersburg alipokutana na kufanya mazungumzo na Watanzania wanaoishi na wanaosoma katika vyuo mbalimbali nchini humo.

Waziri Dk Gwajima amesema kuwa Tanzania ina fursa nyingi za kuwekeza katika sekta mbalimbali katika kusaidia jamii ikiwemo sekta ya afya, utalii na madini ambazo zinaweza kuchangia katika maendeleo ya taifa.

Ameongeza kuwa kuishi au kusoma nje ya Tanzania hakufungi milango kuwekeza nyumbani na kuleta mabadiliko katika Taifa ulilotoka ila ndio linaongeza fursa na nafasi ya kuleta mabadiliko katika jamii kutokana na mambo mapya ya kujifunza kutoka mataifa mengine.

"Niwaambie ndugu zangu nyumbani kumenoga wekezeni nyumbani haijalishi wewe unaishi huku au wewe ni mwanafunzi mnaweza mkajiunga pamoja na kuanzisha umoja wenu mkatafuta wafadhili mkiwa Urusi na mkawasaidia Watanzania wenzenu" amesema Dk Gwajima.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi