loader
Dstv Habarileo  Mobile
Daktari aeleza hatari kuchelewa tiba saratani ya matiti

Daktari aeleza hatari kuchelewa tiba saratani ya matiti

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Dk Julius Mwaisalage ameeleza hatari ya kuchelewa kupata tiba ya saratani ya matiti.

Dk Mwaisalage alisema hayo Dar es Salaam katika mahojiano na HabariLEO. Oktoba ni mwezi wa uhamasishaji na elimu ya saratani ya matiti.

Alisema asilimia 70 ya wanawake hufika hospitali wakiwa katika hatua za juu za ugonjwa hali inayogharimu maisha yao.

Mwaisalage alisema endapo watawahi hospitali katika hatua ya kwanza na ya pili, wagonjwa wanaweza kutibiwa na kupona.

“Saratani zinazoongoza Tanzania ni za aina mbili, kuna ya mlango wa kizazi ambayo inachukua karibia asilimia 35 ya wagonjwa halafu inakuja saratani ya matiti ambayo inachukua asilimia 15 ya wagonjwa,” alisema.

Alisema inayofuata ni ya mlango wa chakula. “Hii wanapata wote, inayofuata ni saratani ya ngozi, inayofuata ni mfumo kichwani, shingoni, mdomoni na ya sita ni saratani ya tezi dume ambayo ni wanaume wanapata tu.”

Dk Mwaisalage alisema wanawake wengi wanaugua saratani kwa sababu ya jinsi yao kutokana na mabadiliko ya vichocheo na mfumo wa maisha yao.

Alihimiza wanawake kuwa na tabia ya kupima afya mapema kwa kuwa saratani ya matiti ikigundulika mapema inatibika.

foto
Mwandishi: Aveline Kitomary

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi