loader
Dstv Habarileo  Mobile
DPP afunguka wingi kesi za wanyamapori

DPP afunguka wingi kesi za wanyamapori

MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP), Sylvester Mwakitalu amesema makosa kuhusu wanyamapori na mazao ya misitu ni tatizo kubwa nchini na kuna kesi nyingi mahakamani.

Mwakitalu alitoa mfano kuwa takribani nusu ya kesi zitakazosikilizwa na jopo la majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania mkoani Mara zinahusu wanyamapori.

Alisema hayo mjini Morogoro wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya upelelezi kwa waendeshaji kesi dhidi ya wanyamapori na misitu.

Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya makosa ya mazingira na maliasili katika ofisi ya DPP, Rosemary Shio alisema mafunzo hayo yanashirikisha wajumbe 57.

Washiriki hao ni mawakili wa serikali wa mikoa yote ya Tanzania, waendesha mashitaka na wapelelezi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Jeshi la Polisi.

Alisema utalii na mapato ya mazao ya misitu na maliasili nyingine yana mchango mkubwa kwa uchumi wa nchi hivyo ofisi ya DPP imeona umuhimu wa kutoa mafunzo kwa wanaoendesha kesi hizo ili kuongeza ufanisi na kulinda maslahi ya taifa.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi