loader
Ugonjwa wa midomo, miguu kwa ng’ombe waathiri soko la nje

Ugonjwa wa midomo, miguu kwa ng’ombe waathiri soko la nje

UGONJWA wa midomo na miguu (FMD) ambao unaathiri mifugo na kusababisha Tanzania kushindwa kupeleka nyama katika baadhi ya nchi za nje  kulingana na masharti yaliyopo kwenye nchi hizo.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo, Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania (RVCT) Dk. Bedan Masuruli amesema ugonjwa huo umekuwa ukiathiri kwa kiasi kikubwa biashara ya nje na kwamba umekuwa ukisababishwa na uwepo wa wanyama pori.

Amesema ni vigumu kudhibiti ugonjwa huo kwa kuwa Tanzania ina kirusi cha ugonjwa huo ambacho hakipo kwenye chanjo ambazo zinaingizwa nchini kutoka nchi za nje kwa ajili ya kudhibiti ugonjwa huo na kwamba kuna virusi aina saba vya ugonjwa huo.

Amefafanua baadhi ya viwanda ambavyo vimepewa vibali vya kusafirisha nyama kwenda ya nchi vinataratibu ya kuweka mifugo karantini kabla ya kuchinjwa ili kujiridhisha mifugo hiyo kutokuwa na ugonjwa wa midomo na miguu ambao hauathiri binadamu.

Akizungumza wakati akihitimisha kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji Mwenyekiti wa kamati hiyo Dk. Christine Ishengoma ameishauri Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuendelea kuisimamia vyema sekta ya mifugo ili iweze kuongeza mapato kwa kuuza mifugo na mazao yake ndani na nje ya nchi.

Pia, amesema ni vyema elimu iendelee kutolewa kwa ajili ya uzalishaji wenye tija kwenye masoko na uvunaji wa mifugo kusudi uzalishaji uwe wenye tija na kwamba mifugo ipo mingi wafugaji hawapaswi kutokuvuna mifugo yao hali ambayo inasababisha pia viwanda vya kuchakata nyama kutopata malighafi ya kutosha.

 

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi