loader
Mtaka achefukwa, agoma kuidhinisha sh ml. 47, ataka ofisi ya Mkurugenzi kujitafakari

Mtaka achefukwa, agoma kuidhinisha sh ml. 47, ataka ofisi ya Mkurugenzi kujitafakari

MADIWANI wa Jiji la Dodoma, wamemchefua Mkuu wa Mkoa huo, nthony Mtaka, ambaye amegoma kuidhinisha fedha kiasi cha Sh. milioni 47 zilizohitajika kutumiwa na Wakuu wa Idara na Madiwani wa Jiji la Dodoma kwenda mkoani Mbeya kufanya ziara ya kujifunza namna ya uendeshaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya usafi.

Akizungumza katika kikao na watumishi wa Jiji la Dodoma, Mtaka  amesema mbali na gharama hizo, kiujumla ziara hiyo haina tija.

Akitoa mchanganuo wa fedha hizo, Mtaka amesema  madiwani 55 waliomba waidhinishiwe bajeti ya Sh milioni 26, watumishi 14 Sh milioni 7.6, usafiri wa kukodi Sh milioni sita na mafuta Sh 5.7.

Amesema madiwani na wakuu hao wa idara walimwandikia barua ya kuomba fedha hizo kwa lengo la kwenda kujifunza kuhusu masuala ya usafi wa mazingira, ukusanyaji wa mapato na namna ya kutokomeza ‘ziro’ mashuleni jambo ambalo amesema linatia shaka.

Amesema wakuu hao wa idara pamoja na madiwani hawakupaswa kufanya hivyo kwani mambo wanayotaka kufuata Mbeya yapo jijini Dodoma.

Ameongeza kuwa fedha wanazohitaji ni nyingi kiasi kwamba zinatosha kujenga madarasa ya kisasa mawili na kubakisha ziada.

“Hivi kweli uchukue hela za madarasa mawili kwa ajili ya ziara ya kujifunza kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako na unaishi nacho? Dodoma kuna miradi mingapi ya kujifunza hapa, kuna utekelezaji wa miradi mingi unaendelea shida ni uvivu wa kufikiria na si vinginevyo,” amesema.

Amesema kitendo hicho ni matumizi mabaya ya fedha za Serikali ambazo zinatokana na kodi za wananchi masikini huku akiongeza kuwa katika maelekezo ya Ofisi yake, Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma inapaswa kujitafakari kuhusu jambo hilo.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi