loader
Makalla atoa maelekezo mapya  maeneo waliyoondoka Machinga

Makalla atoa maelekezo mapya maeneo waliyoondoka Machinga

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri, watendaji wa kata na mitaa wasimamie na kuweka uangalizi wa kutosha maeneo waliyoondoka wafanyabiashara wadogo (Wamachinga).

Alitoa maelekezo hayo jana wakati wa kikao na watendaji kata na mitaa kuhusu tathmini ya kazi ya kuwapanga upya Wamachinga Dar es Salaam.

Alizitaka halmashauri za Dar es Salaam kuzitumia kampuni zilizopewa zabuni ya usafi kwenye maeneo husika kufanya usafi ndani ya wiki moja kwa lengo la kuliweka jiji la Dar es Salaam katika mandhari safi na kuvutia.

Kuhusu wafanyabiashara waliokubali kuvunja vibanda na sasa wanapanga bidhaa zao chini kwenye maeneo yaleyale yaliyokatazwa, mkuu huyo wa mkoa amepiga marufuku utaratibu huo na kuwataka wafanyabiashara hao kwenda kwenye maeneo waliyopangiwa.

Pia amezielekeza taasisi zote za umma zikiwamo shule, vyuo, mashirika, hospitali na nyinginezo kutoruhusu wafanyabiashara hao kufanya biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa na kuzisisitiza Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijini (Tanroads) kuzilinda barabara zao zisivamiwe upya.

Alisisitiza kuwa ifikapo Oktoba 30 asionekane mfanyabiashara yoyote akiendesha biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa na kuwataka kutumia muda wa nyongeza uliotolewa kuyahama maeneo hayo.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/1a9312ed93b4cf66102e76e73ffefc37.jpeg

BODI ya filamu Tanzania imesema maandalizi ya tuzo za ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi