loader
Watumishi Takwimu, watakiwa kuchanja

Watumishi Takwimu, watakiwa kuchanja

MKURUGENZI Mkuu wa ofisi ya Takwimu Tanzania (NBS ) Dk. Albina Chuwa, amesisitiza wafanyakazi wa ofisi hiyo kuchanja ili kujikinga na ugonjwa wa Covid 19

Dk. Chuwa ameyasema hayo leo  Jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa kikao cha tano cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Takwimu.

Alisema ugonjwa huo ni hatari endapo mtu akiupata na gharama zake ni kubwa kujitibu hivyo ni vema watumishi hao wakapata chanjo ili kujikinga na Covid-19

Pia alisisitiza wananchi kujiweka tayari katika zoezi la sensa itakayofanyika mwakani na kutoa rai kwa taasisi binafsi kutumia takwimu za serikali kupata taarifa sahihi za kimaendeleo

Wafanyakazi wa ofisi hiyo wamekutana kwa ajili ya kujadili changamoto zao sanjari na kuboresha huduma bora katika ofisi hiyo pia wanapewa elimu ya ununuzi wa hisa, masuala ya lishe bora pamoja na jinsi ya kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza.

foto
Mwandishi: Veronica Mheta,Arusha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi