loader
Aggy Baby aje na 'Watajuaje'

Aggy Baby aje na 'Watajuaje'

MSANII wa Bongo Movie  ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za kizazi kipya Agnes Suleimani 'Aggy Baby' ameachia ngoma mpya katika tasnia ya music ya Bongo ujilikanao kama  'WATAJUAJE'

Ujio wa 'Utajuaje' unakuwa wimbo wa pili kutoka kwa msanii huyo aliyetamba na filamu mbalimbali za kibongo ikiwepo Pangusa iliyokuwa ikirushwa na kituo cha Televisheni cha Azam.

Mbali na upande huo wa filamu na kibongo, Agnes ambaye pia ni mwandishi wa nyimbo na mshauuri wa vijana katika masuala mbalimbali,  pia aliwahi kutamba na kibao chake kiitwacho 'Wanipa' alichokiachia mwaka jana.

Akizungumzia wimbo huo, Aggy Baby' anasema 'Watajuaje' ni muendelezo wa mikakati yake ya kuhakikisha anaupeleka mbele muziki huo na kutoa burudani ya kutosha kww mashabiki wake.

Amesema muziki kwake ni kazi iliyopo katika damu yake na kusistiza kuwa kwa sasa amejipanga kuachia ngoma moja badala ya nyingine na kuwataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula.

Amewataka mashabiki wake kuusikiliza Watajuaje kupitia platform za Boomplay, tube, itunes pamoja na audiomack.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/9b73862c41883a3311bc38c65bcf404f.jpg

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi