loader
Wahudumu vituo vya afya watakiwa kutoa elimu, kuacha unyanyapaaji

Wahudumu vituo vya afya watakiwa kutoa elimu, kuacha unyanyapaaji

Watoa huduma za afya wametakiwa kutoa elimu kuhusu ualbino na kuacha unyanyapaa kwa wanawake wote wajawazito wanaohudhuria kliniki wakati wa kujifungua. 
 

Rai hiyo imetolewa na Ofisa Ustawi wa Jamii, Wilaya ya Ukerewe, Nasra Msuya ambapo amesema watoa huduma za afya wanapaswa kuwathamini na kuwapa ushirikiano walemavu.
 
Mratibu wa mradi jumuishi wa vyombo vya habari unaotekelezwa na shirika lisilokuwa la Kiserikali la Standing Voice, Chrispine Mabwenga amesema wanaojifungua watoto wenye ualbino hospitalini wanaweza kupata elimu kuhusu ualbino itakayowasaidia.
 
Mabwenga amesema akina mama wengi ni wahanga wakubwa hasa wanapojifungua watoto wenye ualbino. Amesema masuala ya imani potofu yamesababisha unyanyapaa kwa watu wenye ualbino.

Amesema shirika lao litaendelea kutetea haki za watu wenye ualbino kupitia miradi yao mbalimbali ya afya ikiwemo kuzuia na kupambana na Saratani ya ngozi, afya ya macho.

Mabwenga ameongeza kuwa shirika lao litaendelea kutoa elimu  kuhusu uoni hafifu kwa wanafunzi wenye ualbino na walimu.

Naye  Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ulemavu Wilaya ya Ukerewe,Castory Ilungu amesema miaka ya nyuma wilayani Ukerewe kulikuwa na tatizo kubwa la ufukuaji la maiti za watu wenye ualbino na watu walikuwa wakichukua viungo vyao kwa imani za kishirikiana.

Amesema kupitia Elimu mbali mbali za shirika la Standing Voice wameweza kushawishi jamii kuachana na mila za potofu kuhusu ualbino.

foto
Mwandishi: Na Alexander Sanga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi