loader
Tanzania yapanda viwango vya Fifa

Tanzania yapanda viwango vya Fifa

KUFANYA vizuri kwa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia, kumeifanya Tanzania kupanda nafasi mbili juu kutoka nafasi ya 132 hadi 130 katika viwango vya ubora wa soka vilivyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) jana.

Taifa Stars imetoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Benin ugenini katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022 uliochezwa hivi karibuni.

Pia ilishinda dhidi ya Madagascar mabao 3-2 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Benjamini Mkapa na kutoka sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), huku ikipoteza nyumbani dhidi ya Benin kabla ya kwenda kurudiana na kushinda.

Mwezi uliopita Tanzania ilipanda nafasi tatu kutoka 135 hadi 132 na sasa nafasi mbili kutoka 132 hadi 130 ikiwa imepata jumla ya kura 112,384. Benin ambao wako kundi moja na Taifa Stars wanaonekana kushuka nafasi moja kutoka 82 hadi 83, DRC ikishika nafasi ya 67 na Madagascar ikipanda nafasi moja kutoka ya 100 hadi 99.

Katika ukanda wa Afrika Mashariki, Uganda inaendelea kuongoza ikipanda nafasi nne kutoka nafasi ya 

86 hadi 82, Kenya ikishuka kutoka 102 hadi 104, Rwanda ikishuka kutoka 128 hadi 133 na Burundi ikibaki nafasi ya 141.

Bara la Afrika Senegal bado ni kinara ikishika nafasi ya 20 duniani, ikifuatiwa na Tunisia iliyoshuka kutoka 25 hadi 27, Morocco ikipanda kutoka ya 33 hadi 29, Algeria ni ya 30, Misri ikipanda kutoka 48 hadi 44 na Nigeria imeshuka kutoka 34 hadi 36.

Ubelgiji inaendeleaa kuongoza kwa ubora duniani ikifuatiwa na Brazil, Ufaransa na Italia katika nafasi ya nne.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e7dd7d293ececc344fb477a61b5e27f3.jpeg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi