loader
SIMBA YAITA MASHABIKI KWA MKAPA JUMAPILI

SIMBA YAITA MASHABIKI KWA MKAPA JUMAPILI

MAANDALIZI ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na Jwenang Galaxy ya Botswana yamekamilika na wawakilishi hao wa Tanzania wapo tayari kwa mtanange huo ambao utapigwa Jumapili kwenye Dimba la Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kaimu Msemaji wa klabu hiyo, Ally Shatry ‘Chico’ alisema pamoja na ushindi wa mabao 2-0 waliopata ugenini, wanahitaji kupata ushindi mwingine kwenye uwanja wa nyumbani ili kujihakikishia kuingia hatua ya makundi.

“Wageni wetu wamewasili nchini ingawa wamefanya siri, tuna wakaribisha na sisi tumejipanga kuhakikisha tunatumia vema uwanja wa nyumbani kupata ushindi mnono kama ilivyozoeleka tunapokuwa kwenye michuano hii,” alisema Chico.

Alisema kikosi hicho kimeingia kambini juzi na wachezaji wote wapo katika hali nzuri na Nahodha John Bocco na Kocha Didier Gomes wameahidi ushindi wa kishindo baada ya kuwajua na kuwasoma Jwenang Galaxy.

Chico alitambulisha kauli mbiu mpya watakayoitumia kwenye mchezo huo ambayo ni ‘It’s not over kazi iendelee’ na kusema ana amini watashinda mchezo huo na kuendelea kuipeperusha vema bendera ya taifa na kutinga kwa mara nyingine hatua ya makundi kama misimu miwili iliyopita.

Viingilia katika mchezo huo viti vya buluu itakuwa Sh. 5000, mzunguko kwa kununua kwenye mtandao lakini ukinunua uwanjani itakuwa Sh 7000, VIP B, C 20000, VIP A 40000, Platnums 150,000 watakaonunua tiketi hizo watapata vifurushi maalumu vyenye zawadi za Simba pia watapata eskoti kutoka hoteli ya Hyyat hadi uwanjani na uwanjani watapata chakula na vinywaji.

Naye Burton Mwambe ‘Mwijaku’ alisema Simba kwa sasa ndio mabingwa pekee wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na wamejipanga vizuri kuchukua dhamana ya kupeperusha bendera ya taifa katika michuano hiyo mikubwa Afrika.

“Nina uhakika Jumapili Simba itashinda tena kwa idadi kubwa ya mabao na isipotokea hivyo nitatembea uchi wa mnyama kutoka Posta hadi Mwenge na msiponiona uwanjani popote mtakaponiona mnipige mawe mpaka nife,” alisema Mwijaku.

Naye shabiki wa timu hiyo, Kay Mziwanda aliwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi Jumapili kwa ajili ya kuishangilia timu yao ili iweze kufanya vizuri kwani mchezo huo ni mgumu na ili kutinga makundi wanalazimika kushinda.

“Tunamwambia mama kwenye soka nchi ipo salama, tumejipanga, sisi ndio timu pekee ambayo tumeruhusiwa mashabiki 15,000, hilo linaonesha Simba ni timu kubwa. Twendeni tukashangilie timu yetu,” alisema Kay Mziwanda.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d2f3a344c1d0f8998cfc49539da35dc1.png

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi