loader
Washindi NBC Marathon kulamba milioni 69/-

Washindi NBC Marathon kulamba milioni 69/-

ZAIDI ya Sh milioni 69 zimetengwa kwa ajili ya washindi 44 wa NBC Marathon 2021 zitakazofanyika Dodoma Novemba 7.

Mwakilishi wa NBC, William Kallage akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio hizo Dar es Salaam jana, alisema mwaka huu wameongeza zawadi za washindi, ambapo mshindi wa kwanza wa kilometa 42 kwa wanaume na wanawake kila mmoja ataondoka na Sh milioni 5.5.

Alisema kwa upande wa kilometa 21, mshindi ataondoka na kitita cha Sh milioni 3.5, wakati katika kilometa 10, mshindi atapewa Sh milioni 1.5 na wa kilometa tano atapewa Sh milioni 1.

Alisema lengo kuu la mbio hizo ni kuchangia huduma za afya katika Hospitali ya Ocean Road, hasa matibabu ya saratani ya shingo ya kizazi ambayo ndiyo inayoua sana kwa magonjwa ya saratani hapa nchini.

Alisema mwaka jana katika mbio ya kwanza, NBC ilichangia Sh milioni 100 kwa tatizo hilo na mwaka huu wanataka kuchangia fedha zaidi ili kuhakikisha akina mama wengi wanapata matibabu.

Alisema mbali na viingilio vya washiriki, pia wamekuwa wakipata fedha kutoka kwa wafadhili na kutoka kwa wateja wao ambao nao wamekuwa wakichangia.

Alisema mwaka huu wanatarajia kushirikisha zaidi ya wanariadha 3,000 kutoka mikoa yote ya Tanzania, wakati mwaka jana walioshiriki walikuwa 1,944.

Daktari wa Hospitali ya Ocean Road, Crisprin Kahesa alisema saratani ya mlango wa kizazi ndio ugonjwa unaoua zaidi kwa upande wa saratani, hivyo aliomba watu kusaidia kuchangia matibabu hayo. Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho

la Riadha Tanzania (RT), Jackson Ndaweka alisema mwaka huu wamejipanga vizuri kuhakikisha wanaondoa kasoro zote zilizojitokeza katika mbio za mwaka jana.

Aliipongeza NBC kwa kudhamini mbio hizo kwani mbali na kuchangia matibabu ya saratani ya mlango wa kizazi, pia zinasaidia kuuendeleza mchezo huo.

Alisema mbio za mwaka huu zitahusisha pia wanariadha wakubwa kutoka nchi za Kenya, Uganda, Ethiopia na wa Tanzania.

Ndaweka aliwataka wakimbiaji wa Tanzania kujitokeza kwa wingi kushindana, kwani zawadi zimewekwa kwa faida yao.

Mwakilishi wa kampuni ya bima ya Jubilee alisema wataendelea kusapoti mbio hizo na aliwataka wanariadha kujitokeza kwa wingi kushiriki kwani fedha zitakazopatikana zitasaidia matibabu ya akina mama wanaosumbuliwa na maradhi hayo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/9583f6988b8e262f044935e42dac9103.jpeg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: Cosmas Mlekani

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi