loader
Serikali kuendelea kusaidia michezo

Serikali kuendelea kusaidia michezo

SERIKALI imesema itaendelea kusaidia maendeleo ya michezo nchini na imewapongeza wanamichezo wote waliotajwa katika tuzo zilizotolewa juzi.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika usiku wa tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) zilizofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere (JNICC), Dar es Salaam juzi.

Waziri Mkuu alisema serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu wake, Dk Philip Mpango inadhamini michezo ndio maana Rais alidhamini Mashindano ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake kwa nchi za Ukanda wa Cecafa.

“Rais Samia na Makamu wake Dk Mpango wanajali na kuthamini michezo na wanawapongeza wote mtakaopata tuzo usiku huu na Rais wetu Samia anapenda michezo, ndio maana alidhamini Cecafa ya wanawake,” alisema Majaliwa.

Alisema tuzo ni zawadi baada ya kufanya vizuri na zinatoa motisha kuendelea kufanya vizuri na wengine kutamani kupata, hivyo alilishukuru Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kumwalika, klabu na wadhamini, kwani tuzo hizo ni matokeo ya kazi waliyoifanya.

Alitioa rai mwakani nao watambuliwe kwenye tuzo.

“Na wale mtakaopata zawadi, wale walimu… Mimi ni mwalimu mwenzenu natamani na mimi siku moja mkatambua mchango wangu na mimi nikapata tuzo maana nacheza nje, natamani siku moja mkatengeneza kipengele chetu na sisi tukatambuliwa hapa,” alisema Majaliwa.

Pia aliwashukuru wadhamini wa kila klabu na kuwataka kuendelea kufanya hivyo kwani inasaidia kwenye maendeleo ya michezo na kwamba serikali pamoja na TFF inatambua mchango wao.

Baada ya kuwatunukia tuzo wanamichezo waliotajwa, Waziri Mkuu pia alipewa tuzo ya heshima na Rais wa TFF kwa kutambua mchango wake katika michezo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/67cca48a30150c530445564cf0b71533.jpeg

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi