loader
AZAM, BIASHARA KARATA MUHIMU CAF

AZAM, BIASHARA KARATA MUHIMU CAF

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisha Afrika, Azam FC na Biashara United leo wanashuka kwenye viwanja vya ugenini kusaka ushindi ambao utawavusha kwenye raundi ya pili ya michuano hiyo.

Biashara ambayo ilikuwa katika hatihati ya kwenda Libya kurudiana na Al Ahly Tripol kutokana na ukata, ilitarajia kuondoka nchini usiku wa kuamkia leo kwa ndege ya kukodi baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuitaka Kurugenzi ya Michezo na TFF kuhakikisha timu hiyo inasafiri.

Majaliwa alitoa agizo hilo wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo za TFF, ambazo yeye alikuwa mgeni maalumu.

Kwa mujibu wa chanzo kutoka ndani ya timu ya Biashara, timu hiyo ilitarajiwa kuondoka usiku wa kuamkia leo kwa ndege ya kukodi, ambayo hata hivyo haikuelezwa ni ya shirika gani.

“Shirikisho mhakikishe mnaratibu klabu, ambazo zinaendelea na mashindano ya kimataifa kwa sababu ile ni sura ya nchi, Biashara ambayo inatakiwa kucheza kesho kutwa (leo) isimamie iende ikacheze,” alisema Majaliwa.

Alisema baada ya tuzo wakae waone namna, ambayo timu itaondoka kwa sababu anaamini itashinda mchezo huo na hata kama ni kushindwa ikashindwe huko, lakini alisisitiza anaamini itashinda.

Katika mchezo wa awali wa mkondo wa kwanza dhidi ya FC Dikhil ya Djibouti, Biashara iliondoka siku ya mchezo na kuingia moja kwa moja uwanjani, lakini ilishinda kwa bao 1-0.

Awali, Mwenyekiti wa Biashara aliomba kuachwa kwanza, kwani alikuwa akishughulikia namna timu itakavyoondoka, huku Mkurugenzi wa Michezo, Dk Singo naye akisema aachwe kuna jambo analishughulikia alipopigiwa simu jana.

Kikosi cha Azam FC kimeshatua kwenye mji wa Cairo tangu Jumatano usiku tayari kwa mchezo wao huo leo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids, ambapo katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam walitoka suluhu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e9a200cafc0c303625dd2aa647fc2400.jpeg

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi