loader
Simba yafunika tuzo za TFF

Simba yafunika tuzo za TFF

KLABU ya Simba imezoa tuzo kibao za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) msimu wa 2020-21 kwa wachezaji, makocha, waamuzi na viongozi ambao walifanya vizuri.

Hafla ya kukabidhi tuzo hizo ilifanyika juzi katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam, ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuwa mgeni maalumu.

Tuzo hizo ziligawanyika katika makundi matatu ambayo ni Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), na Ligi Kuu ya Wanawake.

Tuzo ya mfungaji bora ilikwenda kwa John Bocco aliyefunga mabao 16 na pia akaibuka mchezaji bora Ligi Kuu. Beki bora alituzwa Mohamed Hussein wa Simba, kiungo bora wa Ligi Kuu Clatous Chama, kipa bora Ligi Kuu ni Aishi Manula ambaye pia alitwaa tuzo ya kipa bora wa ASFC.

Tuzo ya goli bora ilichukuliwa na Charles Sabiyanka wa Tanzania Prisons, mchezaji bora chipukizi Ligi Kuu ni Abdul Seleman wa Coastal Union, tuzo ya Fair Play ni Kibwana Shomari wa Yanga, timu yenye nidhamu ni Coastal Union, kocha bora ni Didier Gomes wa Simba na mhamasishaji bora ni Nick Leonard ‘Bongo Zozo’.

Kwa upande wa tuzo za Ligi Kuu ya Wanawake mchezaji bora chipukizi ni Asha Juma wa Alliance Girls, mfungaji bora ni Aisha Masaka wa Yanga na Amina Ally wa Yanga akiwa mchezaji bora, kipa

bora ni Janeth Shija wa Simba na kocha bora Edna Lema wa Yanga na timu yenye nidhamu ni Ruvuma Queens.

Tuzo ya heshima ya soka la wanawake ilikwenda kwa marehemu Maneno Tamba. Wengine waliopewa tuzo ya heshima ni Leodger Tenga, mchezaji gwiji Abdallah Kibadeni na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa mchango wao wanaotoa kwenye michezo. Waziri Mkuu pia ni kocha wa mpira.

Kwa upande wa tuzo za waamuzi, Ramadhan Kayoko aliibuka mwamuzi bora Ligi Kuu, kwa mara ya pili mfufulizo, mwamuzi msaidizi ni Frank Komba kwa mara pili mfululizo, Amina Kyando mwamuzi bora Ligi Kuu ya Wanawake na Sidhani Mkurungwa akiibuka mwamuzi bora msaidizi.

Tuzo ya mchezaji bora Azam Sports Federation Cup (ASFC) ilichukuliwa na Feisal Salum, Releants Lusajo mfungaji bora, kamishna bora, Billy Mwilima na meneja bora wa uwanja ni John Nzwalla wa Nelson Mandela wa Rukwa.

Kikosi bora cha Ligi Kuu Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Joash Onyango, Dickson Job, Mukoko Tonombe, Clatous Chama, Feisal Salum, John Bocco, Prince Dube na Luis Miquissone.

Kikosi bora cha Ligi ya Wanawake ni Janeth Shija, Julietha Singano, Happy Mwaipaja, Fatuma Issa, Amina Bilali, Stumai Abdallah, Mawete Musolo, Oppah Clement, Aisha Masaka na Dotto Tossi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/3e6af512d51e74b1738686fa6a5e4678.jpeg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi