loader
Polisi yaiengua Yanga kileleni

Polisi yaiengua Yanga kileleni

POLISI Tanzania imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kuishusha Yanga baada ya kuifunga Ruvu Shooting bao 1-0 kwenye  Uwanja wa Mabatini, Pwani jana.

Polisi ilisubiri hadi dakika ya 78 kupata bao hilo lililofungwa na Vitalis Mayanga.

Kwa ushindi huo, Polisi imefikisha pointi tisa sawa na Yanga, lakini ikiongoza kwa uwiano mzuri wa mabao. Zote zimecheza mechi tatu.

Ruvu Shooting inabaki na pointi sita katika nafasi ya nne ikiwa imecheza michezo minne, ikishinda miwili na sare mbili.

Mchezo mwingine ulitarajiwa kuchezwa jana usiku ni kati ya Dodoma Jiji na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena Ijumaa ya wiki hii, ambapo Mbeya Kwanza itacheza dhidi ya Biashara, Yanga na Azam FC Jumamosi  na Simba dhidi ya Coastal Union itachezwa Jumapili.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/4689f2531b304b7513fcbe28809f10db.jpg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi