loader
Majaliwa aimwagia sifa  Wizara ya Sanaa, Michezo

Majaliwa aimwagia sifa Wizara ya Sanaa, Michezo

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameimwagia sifa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo chini ya Waziri, Innocent Bashungwa kuwa  imefanya vizuri na kuitangaza nchi kimataifa katika michezo mbalimbali ikiwamo mpira wa miguu.

Majaliwa alitoa pongezi hizo alipopewa nafasi ya kuzungumza katika hafla ya kuapishwa Waziri wa wizara hiyo, Bashungwa na Naibu wake, Pauline Gekul, Ikulu Dar es Salaam jana.

Katika miezi sita ambayo Rais Samia Suluhu Hassan, akiwa madarakani miongoni mwa mafanikio katika sekta ya michezo ni timu za taifa za wanawake na wanaume kufanya vizuri.

Miongoni mwa mafanikio ni ushindi wa timu ya taifa ya wanaume chini ya umri wa miaka 23 iliyotwaa Kombe la Cecafa nchini Ethiopia na Twiga Stars iliyotwaa taji la Cosafa Afrika Kusini. 

Majaliwa alisema katika kipindi cha awamu ya sita, moja ya wizara zilizofanya vizuri na imeonesha mafanikio makubwa tangu Rais Samia alipoingia madarakani ni wizara hiyo.

“Tumeona ushiriki wa Watanzania katika michezo mbalimbali  pamoja na vikundi vilivyoundwa kwa michezo mbalimbali tumeanza kuona mafanikio katika michezo hasa mpira wa miguu na wanamichezo wanaoshiriki michuano hiyo wanaliletea sifa taifa kwa timu za wanaume na wanawake.”

“Sasa tumeanza kuona timu zetu zinaanza kushiriki michuano ya kimataifa na kufanya vizuri, juzi  nilipata kuhudhuria mkutano mkuu wa tano uliokusanya wabunifu wawekezaji wanaojishughulisha na masuala ya Tehama zaidi ya 800,” alisema Majaliwa.

Alisema yapo mafanikio makubwa ambayo wameanza  kuyaona katika eneo hilo la Tehama ambako kumefungua mlango wa fursa za watu kujiajiri na kuajiriwa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f1a6183fa974025b669c4433f7b01829.jpg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi