loader
Geita Gold yaachana na Ndayiragije

Geita Gold yaachana na Ndayiragije

KLABU ya Soka ya Geita Gold ya mkoani Geita imeachana na aliyekuwa kocha wake mkuu, Etiene Ndayiragije baada ya timu hiyo kushindwa kufanya vizuri kwenye michezo minne ya awali ya ligi kuu ya Tanzania bara.

Katika taarifa yake, klabu hiyo imethibitisha kuchukua maamuzi hayo kwa kile kilichoelezwa ni kocha huyo kushindwa kutumiza malengo waliyojiwekea kwenye mkataba.

Akizungumuzia taarifa hiyo jana kwa waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita ambao ni wamiliki wa timu, Zahara Michuzi amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kikao cha uongozi wa timu.

Zahara amesema tathimini imebaini mbinu za kiufundi za mwalimu hazionyeshi mwelekeo wenye tija kuifanya timu kuwa imara na kufikia malengo ya kuwa miongoni mwa timu bora 10 nchini.

“Siyo kwamba tunalazimisha ushindi, kufungwa kupo, lakini tusifungwe tukarudi tulikotoka, hayo siyo  mategemeo yetu, hatuwezi kukubali,” alisisitiza Zahara.

Zahara ameweka wazi kuwa timu itaendelea kubakia mikononi mwa aliyekuwa kocha msaidizi Felix Minziro hadi pale maamuzi ya kumupata kocha mwingine yatakapofanyika.

Naye Mwenyekiti wa Timu ya Geita Gold, Leonard Bugomola amesema uamuzi haujafikiwa kwa sababu ya shinikizo la mashabiki bali ni uhalisia wa mwenendo mbaya wa timu.

 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/3b4733ac835997d6653ff6bc428d7ab2.jpg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: Na Yohana Shida, Geita

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi