loader
Simba kuwavaa wababe wa Azam FC

Simba kuwavaa wababe wa Azam FC

Klabu ya Simba imepangwa kucheza na Red Arrows ya Zambia katika raundi ya kwanza ya michunao ya Kombe Shirikisho Afrika itakayoanza Novemba 28, 2021 Simba itaanza mchezo wa kwanza katika Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam, ambapo baada ya mchezo huo, Simba itasafiri tena Disemba 5 kuelekea Zambia kwa ajili ya mchezo wa marudiano.

Simba imeangukia katika michuano hiyo baada ya kuondolewa Ligi ya Mabingwa kutokana na kanuni ya mabao ya nyumbani na ugenini ambapo Simba iliruhusu mabao matatu ikiwa nyumbani, licha ya kushinda 2-0 ugenini.

Sio mara ya kwanza kwa Red Arrows kucheza Uwanja wa Mkapa, waliwahi kuwafunga Azam FC, mabao 4-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa 25 Ago 2021

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/06fc64dfb5de97135f857acd90219042.jpg

TAMASHA la muziki wa dansi ...

foto
Mwandishi: Na Rahimu Fadhili

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi