Wakati hali ya utulivu ikiwa bado haijakaa sawa kunako Man United kufuatiwa vichapo mfululizo, kiungo Mfaransa wa klabu hiyo, Paul Pogba amewatuliza mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia “Huu sio wakati wa kujisikia vibaya.”
Katika ‘Post’ yake ya Twitter, Pogba amewatia moyo mashabiki kwa kuwaambia umefika wakati wa kuamka na sio kujisikia vibaya kwani mwanga utaanza kuonekana siku za mbeleni.
“Wakati wa kuamka, kusimama na mwanga utaonekana siku za mbele,”ameandika Pogba na kuambatanisha na picha yake.
Pogba alilambwa umeme katika mchezo wa Jumapili iliyopita ambapo United ilikubali kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Liverpool katika Uwanja wa Old Traffod.