loader
Zidane hana mpango na Man United

Zidane hana mpango na Man United

KOCHA wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane hana mpango wa kufundisha, hivyo Manchester United waendelee na Ole Gunnar Solskjaer.

Zidane ndio anatajwa kutua Old Trafford atakapoondoka Solskjaer. Vyanzo vinasema, Zidane hana mpango wa kurudi kufundisha kwa sasa bali anasubiri muda muafaka.

Vyanzo vinasema, Solskjaer anapambana kunusuru kibarua chake, lakini idadi kubwa ya wachezaji wamepoteza imani nae katika mbinu zake anazotumia kabla hata hawajafungwa mabao 5-0 na Liverpool kwenye Ligi Kuu mwishoni mwa wiki iliyopita.

Aidha, inadaiwa United inamuwania kocha wa zamani wa Juventus, Chelsea na Inter Milan, Antonio Conte.

Zidane, mmoja wachezaji wa zamani walioshinda Kombe la Dunia katika kikosi cha Ufaransa mwaka 1998, ndiye anapewa nafasi kubwa kuiongoza timu ya taifa ya Ufaransa (Les Bleus Didier Deschamps) atakapoachia ngazi baada ya Kombe la Dunia 2022 au Euro 2024.

Zidane, 49, aliondoka Real Madrid msimu uliopita baada ya kumaliza kipindi chake cha pili Bernabeu.

Katika vipindi viwili tofauti akiwa kocha wa Madrid, alishinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mawili ya La Liga, mawili ya Kombe la Dunia ngazi ya klabu na mawili ya Super Cup.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5185e5a9dca9b150d472ce18cff182f1.jpg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi