loader
Rais Samia atoa viwanja kwa wachezaji Twiga Stars

Rais Samia atoa viwanja kwa wachezaji Twiga Stars

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu amekabidhi hati za viwanja kwa wachezaji wote wa timu ya wanawake ‘Twiga Stars’ kama zawadi baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Cosafa nchini Afrika Kusini wiki mbili zilizopita.

Rais Samia ametoa hati hizo alipoialika timu hiyo pamoja na kukabidhiwa kombe hilo leo Oktoba 27,2021 katika Ikulu ya Dar es Salaam.

Akiungumza kabla ya kukabidhiwa kombe hilo, Rais Samia amesema lengo la kutoa viwanja hivyo ni kuwawezesha wachezaji hao kutengeneza maisha yao na kupata sehemu ya kuishi mara baada ya kuachana soka.

“Mchezo huu unategemea nguvu, itafika mahali watachoka, lazima tuwajengee baadaye yao, tukiwapa viwanja na kuwasaidia tofati mbili tatu, huko mbele watahangaika na mengine ila hawatahangaika na pakukaa,”amesema Rais Samia.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/5b99b87d0a67ab67b1812eb1b59e3a8b.jpg

TAMASHA la muziki wa dansi ...

foto
Mwandishi: Na Rahimu Fadhili

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi