loader
Shahidi kesi ya Mbowe abanwa, ajichanganya

Shahidi kesi ya Mbowe abanwa, ajichanganya

UPANDE wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi yenye mashitaka ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu umembana shahidi wa pili upande wa mashitaka na kusababisha ajichangaye.

Jana katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, shahidi huyo Justine Kaaya alionekana kuchanganywa na maswali ya Wakili wa utetezi, Peter Kibatala.

Mbele ya Jaji, Joachim Tiganga, Kibatala alianza alimuuliza shahidi alikutana lini na Mbowe kwa mara kwanza na alijibu kuwa ni Oktoba mwaka jana.

Katika ushahidi wake awali alidai alikutana na Mbowe Mjini Longido Novemba, 20218 wakati mwanasiasa huyo alipokwenda akihitaji Kaaya ampe taarifa za aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya.

Juzi Kaaya aliileza mahakama hiyo kuwa mwaka huo 2018 alikuwa ameacha kazi kwa Sabaya.

Jana Kibatala alipomuuliza alikutana na Mbowe mara ya mwisho lini, alidai ilikuwa mwanzoni mwa Januari mwaka jana.

Wakili Kibatala alimweleza kuwa wakati huo Mbowe alikuwa mahabusu baada ya mahakama kumuondolea dhamana katika kesi iliyokuwa ikimkabili wakati huo.

“Shahidi unafahamu ya kuwa wakati huo unaotaja Mbowe alikuwa Gereza la Ukonga baada ya mahakama kumuondolea dhamani kwa kesi fulani iliyokuwa ikimkabili? Kwa hiyo ulikutana na Mbowe akiwa mahabusu?,” aliuliza Kibatala na Kaaya akadai hafahamu chochote.

Katika uhalisia, wakati aliotaja Mbowe hakuwa mahabusu kama Kibatala alivyodai.

Tukio la Mbowe kuondolewa dhamana lilikuwa Novemba, 2018. Wakati huo alikabiliwa na kesi ya kufanya mkusanyiko usio na kibali katika harakati za uchaguzi mdogo jimbo la Kinondoni na aliachiwa Machi, 2019 muda ambao ni kabla na aliotaja shahidi mahakamani.

Kibatala alimuuliza Kaaya ikiwa hisia zake kwa Mbowe zilikuwa na harufu ya uhalifu baada ya kuzungumza naye alipokwenda kuonana naye Longido, na Kaaya alijibu ‘ndiyo’.

Juzi shahidi huyo alidai Mbowe alimpa na akapokea Sh 300,000 za usumbufu wa kukubali kwenda kuzungumza naye.

“Pamoja na kuwa ulihisi harufu ya uhalifu bado ulipokea hizo laki tatu bila kujali?” aliuliza Kibatala. Kaaya alijibu ‘ndiyo’ na alipotaka kutoa maelezo kuwa alipewa kama pesa ya usumbufu Kibatala hakuyataka maelezo hayo. Kaaya alidai aliamini maneno ya Mbowe kuwa fedha hizo zilikuwa ni za usumbufu na hazikuwa na lengo lingine lolote.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/b4ccf56558ffdfbfbaaaaaad68f6c2b2.jpg

UMOJA wa Vijana wa Chama ...

foto
Mwandishi: Anna Mwikola

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi