loader
Hitimana alia na Simba

Hitimana alia na Simba

KOCHA Mkuu wa Simba Thiery Hitimana, amesema licha ya ushindi walioupata juzi dhidi ya Polisi Tanzania kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara, lakini adui namba moja katika mchezo huo ni mashabiki wao wenyewe.

Katika mchezo huo uliochezwa uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es Salaam, Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0, na kufikisha pointi saba ambazo zimewaweka nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.

Akizungumza na waandishi wa Habari baada ya mchezo huo juzi, Hitimana ambaye amechukua mikoba iliyoachwa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Mfaransa Didier Gomes, alisema timu yake haikucheza alivyotaka na hiyo imetokana na presha kubwa kutoka kwa mashabiki wao wenyewe.

“Mashabiki wetu walikuwa adui namba katika mchezo wa leo (juzi) muda mwingi walikuwa wakiwazomea wachezaji kitu ambacho kilikuwa kinawapunguzia ufanisi wachezaji na kucheza kwa hofu hasa ukizingatia mchezo uliopita dhidi ya Jwenang Galaxy tulifungwa na kutolewa kwenye michuano ya kimataifa,” alisema Hitimana.

Kocha huyo alisema mbali na presha hiyo kutoka kwa mashambiki wao, lakini wapinzani wao Polisi Tanzania, waliwapa upinzani mkubwa kutokana na muda mwingi kucheza kwa kuzuia huku wakifanya mashambulizi ya kustukiza jambo lililomlazimu kubadili mbinu mara kadhaa mpaka wakafanikiwa kupata penalti.

Alisema kwa kuwa walicheza kwenye presha kubwa kutokana na mambo mengi yaliyojitokeza hivi karibuni kitu cha msingi kwao ilikuwa ni kupata ushindi ambao anaamini utarahisisha na kupunguza presha kwa wachezaji na mechi zao zinazofuata kuwa rahisi kwao.

“Nawapongeza wachezaji wangu kwa kujituma naamini kwakua leo (juzi) tumepata funguo na kuchukua pointi zote tatu sina shaka mechi zinazofuata zitakuwa mteremko kwetu,” alisema Hitimana ambaye kabla ya kutua Simba alikuwa akiinoa timu ya Mtibwa Sugar.

Kwa upande wake kocha wa Polisi Tanzania, Malale Hamsini alisema katika mchezo huo wenyeji wao Simba walikuwa na bahati lakini mchezo kwa ujumla ulikuwa mzuri na wenye ushindani ukiacha bao walilofungwa.

“Niwapongeze Simba kwa ushindi bahati ilikuwa upande wao, lakini pia niwapongeze wachezaji wangu kwa kufuata maelekezo niliyowapa kwa usahihi

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c7c445ffe054e46be77ef3fd85bf16a4.jpg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi