loader
STEVEN GERRARD KOCHA MPYA VILLA

STEVEN GERRARD KOCHA MPYA VILLA

KLABU ya Aston Villa imemteua Steven Gerrard kuwa kocha wake kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu akitokea klabu ya Rangers.

Nahodha huyo wa zamani wa Liverpool, mwenye umri wa miaka 41, anawaacha mabingwa hao wa Uskoti baada ya kuwaongoza kutwaa ubingwa wa kwanza wa ligi katika kipindi cha miaka 10 msimu uliopita.

Gerrard anachukua nafasi ya Dean Smith, ambaye alifutwa kazi Jumapili baada ya kush- indwa michezo mitano mfululizo.

Villa inashika nafasi ya 16 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, pointi mbili juu ya eneo la kushuka daraja.

“Aston Villa ni klabu yenye historia na utamaduni mkubwa katika soka la Uingereza na ninajivunia kuwa kocha wake mkuu,” alisema Gerrard.

“Katika mazungumzo yangu na wamiliki wenza Nassef Sawiris, Wes Edens na bodi yote, mipango yao kabambe kwa klabu, ninatarajia kuwasaidia kufikia malengo yao.”

Gerrard alianza kuwa kocha wa ngazi ya juu na timu ya Ligi Kuu ya Scotland na Rangers mwaka 2018, na ameondoka ikiongoza ligi kwa tofauti ya pointi nne wakifuatiwa na wapinzani wao Celtic.
 

BBC Sport Scotland inaelewa kuwa Aston Villa imewalipa Rangers £uro milioni 4.5 kama fidia.
“Steven na wafanyakazi wenzake wame- hakikisha klabu bila shaka iko katika nafasi nzuri leo kuliko ilivyokuwa miaka mitatu na nusu iliyopita,” alisema mkurugenzi wa mi- chezo wa Rangers, Ross Wilson.

“Tuna hamu Rangers izidi kusonga mbele, kuboresha miundombinu yetu na kuifanya klabu ishinde tena.

“Kumekuwa na maeneo mengi ambayo tunatakiwa kusonga mbele, na bado kuna mengi ya kufanywa, lakini siwezi kusisitiza vya kutosha jinsi ilivyo muhimu kuwa na kocha
wa timu ya kwanza ambaye alishiriki kuweka viwango na kusonga mbele shughuli nzima ya mpira wa miguu.” Gerrard alicheza mechi 710 kwa Liverpool, kushinda mataji tisa, na alitumia msimu katika klabu ya MLS LA Galaxy mwaka 2015 kabla ya kustaafu kama mchezaji mwaka uliofuata.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/d6e5fd1e6af5b05e48192ce8b9bdd613.jpeg

PENALTI ya dakika za majeruhi iliyopigwa na mshambuliaji ...

foto
Mwandishi: BIRMINGHAM, England

Post your comments