loader
Al Noor Kassum afariki dunia

Al Noor Kassum afariki dunia

MWANASIASA mkongwe, Al Noor Kassum amefariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 97 na anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Ismailia- Kijitonyama baada ya mwili wake kuagwa katika Msikiti wa Jamatin uliopo Upanga, Dar es Salaam.

Kassum alizaliwa Januari 11, 1924 na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali kubwa serikalini ikiwamo kuwa Waziri wa Fedha na Utawala wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Aliwahi pia kushika wadhifa wa juu katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani kabla ya kurejea nchini na kuhudumu nafasi nyingine mbalimbali kama mshauri.

Kwa mujibu wa Mwanasiasa mkongwe nchini, Profesa Mark Mwandosya, Kassum wakati wa uhai wake alichangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya nishati na petroli nchini na alilitumikia taifa katika nafasi mbalimbali kubwa ikiwamo uwaziri ambapo aliwahi kuwa waziri mwenye dhamana ya kushughulikia rasimali.

Mitandao mbalimbali ya kijamii jana ilimuelezea Kassum kuwa ni mtu aliyechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa nishati ya petroli na kati ya mambo atakayokumbukwa nayo ni pamoja na kumshauri Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kufanya utafiti kubaini uwapo wa nishati ya petroli nchini ambapo matokeo yake nchi ilibaini uwapo wa madini mbalimbali maeneo ya Kanda ya Ziwa.

Kassum pia atakumbukwa kwa kutumia maarifa makubwa katika kuzuia nishati ya petroli iliyokuwa imeagizwa kutoka nje na aliyekuwa Rais wa Uganda, Iddi Amin kushindwa kuingia nchini humo kitendo ambacho kilisaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza nguvu ya taifa hilo kupambana na Tanzania katika kuelekea Vita vya Kagera.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/3b497b5bc80b020a5c0ba8fd2bc94fe1.jpeg

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka vijana wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi