loader
Liverpool kuijaribu Arsenal, Solskjaer presha juu

Liverpool kuijaribu Arsenal, Solskjaer presha juu

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa Arsenal ya mabadiliko wakati wasakaji hao wa taji la Ligi Kuu watakapokuwa wenyeji wa vijana wa Mikel Arteta katika mchezo utakaofanyika leo.

Kwa upande mwingine, baada ya kumalizika kwa mapumziko kupisha mechi za timu za taifa, Kocha Ole Gunnar Solskjaer akiwa na kikosi chake cha Manchester United leo watakuwa uwanjani ugenini kucheza dhidi ya Watford.

Gwiji wa Liverpool, Steven Gerrard amerudi katika Ligi Kuu na sasa atakuwa na kibarua cha kwanza wakati Aston Villa ikikabiliana dhidi ya Brighton.

ARSENAL Vs LIVERPOOL Tangu walipochakazwa kwa mabao 5-0 huko Manchester City Agosti, Arsenal imejiimarisha na kuwa moja ya timu zilizopo katika kiwango cha juu katika Ligi Kuu ya England.

Kipigo hicho kilitishia kibarua cha kocha wa the Gunners, Mikel Arteta, lakini ukosoaji dhidi yake ulizimwa na ushindi wa mechi nane za ligi bila kufungwa na sasa anaonekana kama mmoja wa makocha bora.

Hata vinara Chelsea hawajawahi kuchukua pointi nyingi katika kipindi hicho kama ilivyofanya Arsenal ambayo imeshinda mechi sita na kutoka sare mbili na 

kupanda hadi katika nafasi ya tano ya msimamo wa ligi hiyo.

Ikitiwa nguvu na kiungo chipukizi wa England, Emile Smith Rowe na mafanikio ya Arteta kuipangua beki yote ya awali iliyokuwa ikivuja, Arsenal sasa inaota kurejea katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kumaliza katika nafasi nne za juu.

Nahodha wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang amerejea miongoni mwa wapachika mabao na kuifanya timu hiyo sasa kuzidi kujiamini zaidi.

“Mimi ni nahodha mtulivu katika ligi, labda duniani,” alisema Aubameyang na kuongeza:

“Kusema ukweli najaribu kuwa mfano. Nafikiri ni sehemu muhimu sana kuwa nahodha.”

Baada ya kurejea kwa mechi za ligi, Liverpool ni tishio kubwa kwa Arsenal, huku vijana hao wa Klopp wakitaka kurudisha matumaini baada ya kufungwa na West Ham kwa mabao 3-2 kabla ya mapumziko kupisha mechi za kimataifa.

Ikiwa pointi nne nyuma ya Chelsea na mbili juu ya Arsenal, Liverpool iliyopo katika nafasi ya nne haitakubali kurudishwa nyuma tena baada ya mechi mbili za ligi bila kupata ushindi.

SOLSKJAER APAMBANA Ole Gunnar Solskjaer amekuwa akipambana ili kutetea kibarua chake Manchester United na akijaribu kuirejesha 

timu hiyo katika mstari itakapocheza dhidi ya Watford.

Kocha huyo anatarajia kufukuzia ubingwa tangu timu hiyo ilipofanya hivyo kwa mara ya mwisho mwaka 2013 baada ya msimu huu kusajili wachezaji wenye majina makubwa kama Cristiano Ronaldo, Jadon Sancho na Raphael Varane.

Ratiba ya leo Jumamosi: A.Villa v Brighton Burnley v Crystal Palace Leicester v Chelsea Liverpool v Arsenal Newcastle v Brentford Norwich v Southampton Watford v Man United Wolves v West Ham

Kesho Jumapili: Man City v Everton Spurs v Leeds

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8720d3e9896c39e176816dd762a4111e.jpeg

PENALTI ya dakika za majeruhi iliyopigwa na mshambuliaji ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi