loader
CRDB Kufungua Tawi Lubumbashi DRC

CRDB Kufungua Tawi Lubumbashi DRC

BENKI ya CRDB imesisitiza kuwa itafungua tawi jipya jijini Lubumbashi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwakani ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa Tanzania na wa DRC kupata mtaji hasa mikopo ya kuendeleza biashara zao ikiwemo kilimo.

Mkurugenzi Mtendaji Benki CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema benki yake imefarijika na taarifa za serikali kufungua ghala kubwa la chakula kwa kuwa itaongeza masoko kwa mazao yanayolimwa zaidi nchini.

“Sisi kama taasisi ya fedha tunatambua kua mkulima bado anachangamoto nyingi lakini kubwa zaidi ni uhakika wa masoko,” amesema Nsekela katika Mjadala wa Kitaifa kuhusu mchango wa Diplomasia ya Uchumi na Mahusiano ya Kimataifa katika kuchochea fursa za maendeleo kwa wananchi kupitia sekta ya kilimo nakuongeza kuwa mpango wa CRDB nikumuwezesha mkulima na mfanyabiashara kunufaika na shughuli zake.

 

Banki Kuu ya Tanzania (BoT) ilitoa idhini kwa CRDB mwezi Mei mwaka huu kuendelea na mpango wake wa kufungua tawi katika nchi jirani ya Kongo.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/5c14375a13b07023097cbbd1df689784.jpeg

WAKALA wa Usafi ri wa Mabasi ...

foto
Mwandishi: NA MWANDISHI WETU

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi