loader
watanzania watakiwa kuchangamkia fursa

watanzania watakiwa kuchangamkia fursa

WATANZANIA wametakiwa kuchangamkia fursa ya kununua gari la kisasa aina ya Nissan Navara ambalo lina uwezo wa kutumika katika matumizi mbali mbali huku likiwa na ubora wa kutosha.

Hayo yamesema jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya magari ya Nissan Tanzania, Christopher Henning katika uzinduzi wa gari hilo.

Amesema gari hilo ni la kwanza kuwepo hapa nchini na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa hiyo kwa kuwa gharama zake ni nafuu.

"Leo tunazindua gari aina ya Nissan Navara ambapo toleo lake ni la mwaka 2021 na gharama zake ni nafuu ambazo ambapo kila mtanzania anauwezo wa kumudu, na kumuwezesha kufanya shughuli zake kutokana na kuwa na ubora halisi "alisema

Henning alisema kampuni hiyo imekuwa ikitengeneza magari yenye ubora wa kukidhi viwango vya juu ambapo pindi mtu anapotumia magari hayo hawezi kununua mara kwa mara.

Kwa upande wake, Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo, Alfred Minja alisema kampuni hiyo imekuwa ikifanya Mapinduzi makubwa katika sekta usafirishaji kwa kutengeneza magari ambayo yana ubora wa kutosha.

Alisema kutokana na matumizi ya kila siku gari aina ya Nissan Navara itamsaidia muhusika kusafiri salama na kufanya kazi zake bila wasiwasi aina yoyote.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5c3aeaf4f643e0bd79b0ee7d11451a6c.jpg

WAKALA wa Usafi ri wa Mabasi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi