loader
Kilimo sayansi ndio majibu ya kujikwamua

Kilimo sayansi ndio majibu ya kujikwamua

MAENDELEO katika sekta ya kilimo ni muhimu hasa katika kukuza uchumi wa taifa na kuleta msukumo kwenye ukuaji wa sekta ya viwanda.

Ukuaji wa sekta ya kilimo una umuhimu mkubwa katika kuzalisha chakula cha kutosha ili kuhakikisha uwepo wa usalama wa chakula na lishe kwa wananchi wakati wote.

Kiukweli sekta ya kilimo kwa miaka ya karibuni inachangia takribani asilimia 29.1 ya pato la taifa, asilimia 65 ya ajira, asilimia 65 ya malighafi inayotumika katika sekta ya viwanda na asilimia 30 ya pato la bidhaa zinazouzwa nje ya nchi. Na ndio maana hata Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda anapotembelea Uganda tunaelewa ana nia gani hasa anapozungumza masuala ya kilimo cha pamoja na matumizi ya teknolojia.

Ni kweli tuna shida nalazima tujifunze kwa wenzetu hasa katika patashika ya kuwa na mafuta ya kupikia ya kwetu wenyewe. Lakini ni dhahiri kutokana na nchi kuingia katika uchumi wa kati wa chini, miaka ya karibuni na hadi sasa taifa linapohangaika kusaka mafuta tukumbushane tu kwamba ni lazima kuendesha kilimo sayansi ili kuinua wakulima wadogo kama tunataka kufanikiwa.

Kwa mujibu wa takwimu za wizara ya kilimo za mwaka 2019/2020 asilimia 90 ya ardhi ya Tanzania hulimwa na wakulima wadogo na hili hatuwezi kulikwepa. Tunaweza kuwa tunaamini katika wakulima wakubw a kunyanyua wadogo lakini yaliyoelekezwa kuendeleza sekta ya Kilimo, katika Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya pili (ASDP II) yenye lengo la kuleta mageuzi ya Sekta ya kilimo (kilimo, mifugo na uvuvi) huwezi kukwepa ukweli wa wakulima na wafugaji wadogo kupewa dozi kamili ya kilimo sayansi.

Mimi naami I ili kuongeza uzalishaji na tija, kufanya kilimo kiwe cha kibiashara zaidi na kuongeza pato la wakulima wadogo kwa ajili ya kuboresha maisha yao lazima kuzingatia mikakati yote ya Taifa: Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025; Mpango wa Maendeleo wa Muda Mrefu (2012-2021); Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016- 2021); Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo (2015) na Mpango wa Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo (Tanzania Agriculture and Food Security Investment Plan – TAFSIP 2011) kila kunapokucha.

Mimi naona kwamba ipo haja ya kuendelea na ajenda ya mageuzi ya sekta ya kilimo kwa kuzingatia kilimo sayansi katika Mnyororo wa thamani wa mazao ya kipaumbele na ikolojia ya kanda ya kilimo. Mageuzi katika kilimo hayajaanza leo kwani hata Mwaka 1972, Mwalimu Julius Nyerere akiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alitangaza Azimio la Iringa lililokuwa na kauli mbiu ya Siasa ni Kilimo.

Tafsiri ya Azimio la Iringa ni kwamba nguvu kazi na ardhi ni muhimu katika maendeleo ya kilimo nchini. Kipindi hicho sekta ya kilimo ilikuwa inakua kwa asilimia nne, ikiajiri asilimia 75 ya Watanzania, wengi wao wakiwa ni wakulima wadogo.

Ukiangalia mwenendo wa kilimo, Serikali zote zilizotangulia hadi awamu hii ya sita imejitahidi kuhamasisha kilimo kwa kuwaandaa wataalamu sasa ni wakati wa kutumia wataalamu wetu kwa ufanisi mkubwa kwa kuwapa nyenzo na nafasi ya kubutua ili kuwaokoa watanzania.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/0f223d72cd09449dad26f7360a62785b.jpeg

KATIKA ukurasa wake wa habari za kimataifa ...

foto
Mwandishi: Na Beda Msimbe

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi