loader
Serikali yapongeza UNESCO kupaisha Kiswahili

Serikali yapongeza UNESCO kupaisha Kiswahili

SERIKALI ime- lipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kutangaza kuwa Julai 7 kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Akizungumza Dar es Salaam jana Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa alise- ma lugha ya Kiswahili kwa sasa inazungumzwa na watu milioni 200 duniani kote na kupongeza Unesco kuipa lugha ya Kiswahili siku yake pekee.

“Tunapongeza Umoja wa Mataifa na Unesco kwa kutambua umuhimu wa lugha ya Kiswahili na kuipa siku yake pekee. Kiswahili kinazungumzwa na watu zaidi ya milioni 200 duniani kote,” alisema Bashungwa.

Bashungwa pia alivi- pongeza vyombo na taasisi zinazosimamia ukuaji wa lugha ya Kiswahili na kuse- ma wanakuja na mpango mkakati wa miaka 10 wa namna lugha itakavyoen- delea kukua na kusaidia kwenda kwa kasi.

“Mpango mkakati huo tunatarajia kuuzindua hivi karibuni na utaanza mwakani hadi mwaka 2032,” alisema Bashungwa.

Unesco ilitangaza siku ya Kiswahili kuadhimishwa kila Julai 7 duniani kote Novemba 23 kwenye makao makuu yake Paris, Ufaransa wakati wa mku- tano wa nchi wanachama wa shirika hilo.

Azimio maalumu la kui- tangaza siku ya Kiswahili lilipitishwa na wanachama wote bila kupingwa.

Hatua hiyo inafanya lugha hii kuwa ya kwanza ya Kiafrika kutambuliwa na Umoja wa Mataifa na kuwa na siku maalumu ya kuadhimishwa.

Kiswahili kinatambulika kama miongoni mwa lugha rasmi kwenye Muungano wa Afrika na kinatumika kama lugha rasmi kwenye Jumuiya ya Afrika Mashari- ki na Bunge la Afrika. Pia ni moja ya lugha za Afrika zinazozungumzwa na watu wengi duniani.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/1c451bf3f622ec5744420eb9277bcb4c.jpeg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Na Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi