loader
Mikakati kuwekwa ‘drones’ zisilete madhara

Mikakati kuwekwa ‘drones’ zisilete madhara

KURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari, amekitaka Chama cha Waongoza Ndege Tanzania (TATCA) kuandaa mikakati ya namna gani wanaweza kutumia ndege zisizo na rubani ‘drones’ katika anga la chini kwa shughuli za kiuchumi.

Alisema hayo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa TATCA, Dar es Salaam jana.

Johari alisema ndege zisizo na rubani ni teknolojia mpya kwa kuwa ilizoeleka tangu zamani anga kutumika na ndege za kawaida za abiria.

Alisema imebainika anga la chini linaweza kutumika kwa shughuli za kiuchumi kwa kutumia ndege zisizo na rubani ikiwemo kubeba vifurushi vidogo vidogo, dawa na kupiga picha.

“Kwa hiyo sisi kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hatutakiwi kuizuia teknolojia, tunatakiwa tuikari- bishe teknolojia lakini tuje na mikakati ya kuona namna gani tutafanya kazi na teknolojia hii ya ndege zisizo na rubani ili zisihatarishe matumizi ya ndege nyingine,” alisema Johari.

Alisema suala la ndege zisizo na rubani limekuwa likizungumzwa mara nyingi na limewekewa utaratibu wa kisheria ikiwemo kusajiliwa, kuwapa mafunzo watumiaji.

Alisema pia ni lazima iwepo teknolojia ya kujua kama mhusika amekiuka kwa kuruka juu zaidi ukomo uliowekwa na hatua za kuchu- kuliwa.

Johari alisema kama ndege zisizo na rubani zikiruka bila utaratibu kwa kuzidi ukomo uliowekwa zinaweza kufyonz- wa kwenye injini ya ndege za abiria na kuleta madhara makubwa.

Alitaka TATCA kujadili kwa kina suala hilo kwa maslahi ya uchumi wa nchi. Rais wa chama hicho cha wa- ongoza ndege, Shukuru Nziku, alisema lengo la mkutano huo wa siku mbili ulioanza jana ni kuwakutanisha wanachama wote nchini na wa nchi jirani kujadili namna ya kuboresha huduma ya kuongoza ndege.

Kaulimbiu ya mkutano huo wa mwaka huu ni ‘waongoza ndege wamejitoa kwa ajili ya usalama wako.’ “Majadiliano yetu kwa mwaka huu yatalenga usalama wa ndege, hivyo tutajadili kuhusu mafunzo, namna ya kubore- sha taratibu za uongozaji wa ndege na mengineyo,” alisema Nziku.

Rais wa Chama cha Waon- goza ndege wa Kenya (KATCA), Maureen Isika, alisema mkutano huo ni muhimu ku- wawezesha kujadili masuala yanayohusiana na usalama iki- wemo kujua hatari zinazoweza kutokea na kukuza utamaduni wa usalama.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Waongoza ndege cha Uganda (UGATCA), Tonny Ssenkubuge, alisema waongoza ndege wana wajibu wa kuweka anga salama na kutoa huduma.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/0c4f95752817c7862ea07a972aa9efb1.jpeg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Na Matern Kayera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi