loader
Viongozi, wanafunzi 2,000 wafunzwa maadili

Viongozi, wanafunzi 2,000 wafunzwa maadili

ZAIDI ya viongozi na watendaji 2,000 kutoka taasisi mbalimbali na wanafunzi wamepata mafunzo ya uongozi na maadili kutoka kwenye Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere cha Dar es Saalam yanayowawezesha kufanya majukumu yao kwa kuzingatia miiko na maadili ya taifa.

Mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila alisema hayo wakati wa mahafali ya 16 yaliyofanyika chuoni hapo ambapo zaidi ya wanafun- zi 4,000 wamehitimu kozi mbalimbali.

Mwakalila alisema idadi hiyo ni utekelezaji wa malengo ya chuo hicho waliyojiwekea mwaka huu. Pia kimefanikiwa kuongeza udahili wa wanafunzi na katika kampasi hiyo ya Kivukoni udahili umeongezeka kutoka wanafunzi 9,754 mwaka 2019/2020 hadi 10,032 mwaka 2020/2021.

“Aidha, katika kampasi ya Karume iliyopo Zanzibar udahili pia umeongezeka kutoka wanafunzi 1,659 mwaka 2019/2020 hadi 2,161 mwaka 2020/2021,” alisema na kuongeza kuwa na Tawi la Pemba limekuwa na wana- funzi 125 katika mwaka 2020/2021.

Alisema kwa ongezeko hilo, idadi ya wanafunzi sasa ni 12,318 kwa mwaka wa masomo 2020/2021.

“Kazi ya kuandaa mitaala mipya na kuhuisha mitaala ya zamani inaendelea ili kuwa na mitaala inayozingatia mahitaji halisi ya kitaifa na kimataifa,” alisema.

Mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi wa chuo hicho, Stephen Wassira alikipongeza chuo hicho kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika utekelezaji wa majukumu yake.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/264fac5a64f9bf6d17acfeb437d403b2.jpeg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Na Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi