loader
Mzumbe kutekeleza mkakati kuinua taaluma

Mzumbe kutekeleza mkakati kuinua taaluma

CHUO Kikuu Mzumbe cha mkoani Morogoro kinaendelea kutekeleza mpango mkakati wa miaka mitano ijayo unaolenga kuinua taaluma na uboreshaji wa miundombinu ya kujifunzia na kufundishia kulingana na upatikanaji wa fedha.

Pia kinaendelea kujitathmini ili kuona taaluma inayotolewa kama bado inahitajika kwenye ulimwengu ambao wahitimu wa chuo hicho wanahitajika kwenda katika ushindani wa soko la ajira na kujiajiri.

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Lughano Kusiluka alisema hayo juzi kwenye mahafali ya 20 mbele ya Mkuu wa Chuo Kikuu hicho na Rais Mstaafu wa Serikali ya Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, kabla ya kutunukia wahitimu shahada mbalimbali zikiwemo za uzamivu (PhD).

Kusiluka alisema kwa kutambua hilo, mwaka huu chuo kilifanya kazi ya kuwafuatilia wahitimu wao na kuzungumza na waajiri kujua wanafundisha nini na soko linahitaji nini.

“Hivi sasa tunaendelea kukamilisha ripoti hiyo na baada ya ripoti hiyo itatusaidia kupitia mitaala yetu na kuifanyia maboresho kulingana na mahitaji ya soko,” alisema.
Kusiluka alisema serikali 
pia imekiwezesha kifedha chuo hicho kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimba- li ukiwemo mradi mkubwa wa elimu ya juu na mageuzi ya kiuchumi iliyotolewa na serikali.

Alisema serikali imekiwezesha Chuo Kikuu kwenye mradi unaosimamiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kukitengea takribani dola za Marekani milioni 21 ambazo ni takribani Sh bilioni 49.

“Kwa hatua hii napenda kumshukuru Rais Samia Su- luhu Hassan na serikali yake kwa uwekezaji huu mkubwa wa miundombinu kwenye elimu ya juu. Ni uwekezaji wa kihistoria,” alisema.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu hicho, Profesa Bernadeta Killian alisema sekta ya elimu bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/c26d43df8423f9fe25618fd29feb5410.jpeg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Na John Nditi, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi