loader
Wakandarasi taka ngumu waomba mikataba iboreshwe

Wakandarasi taka ngumu waomba mikataba iboreshwe

MOJA wa Wakandarasi wa Taka Ngumu Tanzania (UWATANGUTA) umeiomba serikali kuwaboreshea mikataba wanayoingia kufanya nao kazi kutoka mwaka mmoja hadi miaka mitatu ili waweze kukopesheka benki.

Aidha, wamehimiza umuhimu wa serikali kuwashirikisha katika kampeni zinazoendelea za usafi wa mazingira kwa kuwa wao ni wadau muhimu.

Wakizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi, baadhi ya viongozi wa Uwatanguta walisema mikataba mingi wanayoingia na halmashauri mbalimbali ni mifupi, inawanyima fursa ya kukopesheka benki kwa kuwa haiendani na muda
wa marejesho.

Mmoja wa viongozi ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni Investment, Ntuli Damson alisema changamoto wanayokutana nayo ni kuingia mkataba wa mwaka mmoja ambao hautoshi kulipa mkopo wanaopewa benki kuendesha shughuli hizo. mikataba unasababisha hata kushindwa kufanya uwekezaji kwenye teknolojia za kisasa kama kununua magari ya kisasa ya kuzoa taka na hivyo hulazimika kutumia magari chakavu au mabovu.

Mwenyekiti wa Uwatanguta, Mary Ramadhan alisema kuna umuhimu mikataba wanayopewa iwe na masharti mepesi na kwamba wapewe muda wa kusoma mazingira wanayotakiwa kusimamia kwa usafi.

Alitaja changamoto nyingine ni ucheleweshaji wa malipo kutoka katika halmashauri na taasisi mbalimbali. Alisema kuna wakati wanakaa mwaka hadi miaka miwili kiasi kwamba wanashindwa kulipa mishahara kwa watu waliowaajiri.

“Kampuni yetu binafsi halafu malipo kutoka kwa wateja wetu yanachelewa, sasa unapokwenda kuko- pa benki mamilioni ya fed- ha kuendesha shughuli na unarejesha kuanzia miaka miwili, kabla hujamaliza kulipa mkataba unakuwa umeisha,” alisema.

 

Mary alisema kuna haja ya mamlaka kuhama sishwa uchangiaji wa ada za taka kwa mujibu wa sheria kurahisisha utendaji kazi.

Makamu Mwenyekiti wa umoja huo, Abeid Kisinini alisema wakandarasi wakishirikishwa katika kampeni za usafi itakuwa rahisi kush- iriki kikamilifu kwani wao ni wadau muhimu katika mazingira.

Katibu wa Uwatanguta, Elfrida Yairo alisema kuchelewa kwa malipo kumewakimbiza vijana wengi kwenye kazi za usafi. Alisema ndio maana wamekuwa wakifanya kazi na watu wenye umri mkubwa hasa wanawake kwa kuwa ni wavumilivu.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/99f9114e96a149fabfd510cb69e18947.jpeg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Na Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi